
Shiriki picha, video, madokezo ya sauti na maandishi na watu wako kwenye Hali ya WhatsApp. Binafsisha kwa kuongeza vibandiko, GIF na zaidi. Zitapotea kwenye mwonekano baada ya saa 24.













Kwa vibandiko, avata, GIF na maandishi tandazo, una chaguo zote za ubunifu kiganjani mwako ili kuweza kujieleza, kuwa mbunifu na kushiriki uhalisi wako.
Endelea kujulisha kila mtu unayempenda na umtaje katika hali yako wakati una kitu ambacho ungependa aone. Anaweza kuipenda na kuijibu ili kuanzisha mazungumzo.
















Hali yako ni yako ya kushiriki. Ukichapisha, unaamua ni nani anayeweza kuiona, kwa hivyo unaweza kushiriki matukio yako ya nyuma ya pazia kwa amani ya ziada ya kiakili.

Shiriki picha zako za likizo unazopenda zaidi, onyesha ubunifu wako wa hivi karibuni zaidi wa jikoni, au nasa kile kinachoendelea kwa sasa.

Ongeza vibandiko, GIF na maandishi ili kuipa kila hali mguso wa kibinafsi.

Taja watu katika hali yako ili uwafahamishe kwamba umeshiriki kitu. Hawatakosa kitu chochote na wanaweza kukishiriki upya.

Chagua watu ambao unataka kushiriki hali yako nao. Kuanzia waasiliani wako wote hadi marafiki zako wa karibu na familia yako pekee, una udhibiti.






